Ajira na Maendeleo ya Taaluma
Kutoka viwanda vya chakula hadi mashambani — jenga taaluma inayolisha taifa
Zaidi ya Chakula cha Mifugo
Tunajenga mnyororo wa thamani wa chakula wa Tanzania kutoka mwanzo — na tunahitaji watu wanaotaka kujenga kitu cha kudumu.
Kazi yako ina mchango
Kila nafasi ya kazi katika Backbone inachangia maendeleo ya ufugaji na upatikanaji wa chakula nchini Tanzania. Iwe unafanya kazi katika lishe ya mifugo, uzalishaji au usafirishaji, mchango wako unawasaidia wafugaji na familia nyingi.
Fursa za kukua
Tukiwa mzalishaji anayeongoza wa chakula cha mifugo nchini Tanzania, tunaendelea kupanua shughuli zetu kupitia maghala mapya, bidhaa mpya na kufikia maeneo zaidi. Ukuaji huu unaleta nafasi za kazi na fursa za wafanyakazi kujiendeleza.
Mazingira bora ya kazi
Tunaamini wafanyakazi hufanya vizuri wanapoheshimiwa, kusaidiwa na kupewa nafasi ya kutumia uwezo wao. Tunahimiza ushirikiano, kubadilishana mawazo na kutatua changamoto kwa pamoja.
Kua Pamoja Nasi
Tunawekeza katika maendeleo ya wafanyakazi wetu katika kila hatua ya taaluma zao.
Jenga msingi wako
Utapata maelekezo ya kazi, msaada kutoka kwa wafanyakazi wenye uzoefu na mafunzo ya vitendo. Utajifunza hatua za uzalishaji wa chakula cha mifugo, kuanzia malighafi hadi bidhaa kumfikia mfugaji, pamoja na mchango wa nafasi yako.
- Mafunzo maalumu kwa wafanyakazi wapya.
- Mshauri wa kukuongoza katika siku 90 za kwanza.
- Fursa ya kujifunza kazi za idara mbalimbali.
Ongeza ujuzi na uwezo wako
Utapata nafasi ya kusimamia miradi, kuongoza timu ndogo na kuongeza utaalamu wako. Tunawapa wafanyakazi wetu kipaumbele katika nafasi za kupandishwa vyeo. Viongozi wengi wa timu zetu walianza katika uzalishaji au kazi za uwandani.
- Kupandishwa vyeo ndani ya kampuni.
- Bajeti ya kusaidia maendeleo ya kitaaluma.
- Kushiriki mafunzo na makongamano ya sekta.
Ongoza na kuwajenga wengine
Katika hatua hii, utashiriki kuongoza idara, kutekeleza mikakati na kuwaendeleza wafanyakazi wengine. Pia utasaidia kujenga mifumo inayowezesha kampuni kukua.
- Mafunzo ya uongozi.
- Kushiriki katika maamuzi kuhusu mwelekeo wa kampuni.
- Kuwashauri na kuwaendeleza wafanyakazi wengine.
Tutumie Wasifu Wako wa Kazi
Tunatafuta watu wenye uwezo na wanaoshiriki maadili yetu. Tuma wasifu wako wa kazi pamoja na barua fupi ya maombi. Tutawasiliana nawe nafasi inayolingana na uwezo wako itakapopatikana.